vendredi 18 janvier 2013

Rwanda yapinga mpango wa UN kutumia Ndege maalum za uchunguzi dhidi ya waasi wa DRC

     
Marais Joseph Kabila-Kulia, Paul Kagame na Yoweri Museveni-Katikati wakiwa Kampala Uganda
REUTERS/Presidential Press Unit/Handout

Na Victor Robert Wile
Rwanda haitaunga mkono mpango wa Umoja wa Mataifa kutumia Ndege maalum za uchunguzi zisizo na marubani dhidi ya Waasi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaondeleza vitendo vya uasi.
Nchi ya Rwanda haitaunga mkono matumizi ya ndege hizo mpaka pale utakapotolewa ufafanuzi juu ya maswali yao kuhusu namna ambavyo zoezi hilo litakavyotekelezwa.

Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Louise Mushikiwabo ameeleza kuwa ametoa msimamo huo wa nchi yake huku kukiwa na maswali ya kwa nini Rwanda haiungi mkono hatua hiyo.

Umoja wa Mataifa hivi sasa una mpango wa kuliongezea nguvu jeshi lake la kulinda amani nchini Kongo ambako hivi sasa Waasi wa M23 wamedhibiti eneo la jimbo la kaskazini eneo lililo mpakani mwa Kongo na Rwanda.

Muungano wa Mashirika ya kiraia katika Jimbo la Kivu ya kaskazini unaeleza uamuzi wa Rwanda kutounga Mkono mpango wa Umoja wa Mataifa unatokana na uoga wa Rwanda kufichuliwa kile ambacho imekuwa ikikifanya nchini DRC.

Katika ripoti mbalimbali zilizotolewa na Umoja wa Mataifa, Rwanda chini ya Rais Paul Kagame imekuwa ikitajwa kuhusika na harakati za kuwasaidia waasi wa M23 kupambana namajeshi ya Serikali ya Joseph Kabila huku Uganda nayo ikigusiwa kuhusika.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire