mardi 15 janvier 2013

Maandalizi ya kombe la mataifa ya Afrika yakamilika huko Afrika Kusini


Vijana wa timu ya taifa ya DRCongo leopards
Vijana wa timu ya taifa ya DRCongo leopards

Na Victor Robert Wile
Wakati viongozi wa kamati ya maandalizi ya kombe la Mataifa barani Afrika wakitangaza kukamilika kwa shughuli za maandalizi ya michuano hiyo, Waziri wa vijana michezo na utamaduni nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRCongo Baudouin Banza Mukalayi Sungu ameahidi kuwa wachezaji wa timu ya taifa ya DRCongo les Leopards wataoshiriki michuano ya CAN huko Afrika Kusini watapewa posho kabla ya kuanza kwa michuano hiyo. Mbali na hayo waziri huyo amesema madai yote wanaotetea kwa sasa yatapatiwa jawabu pindi tu watakuwa wamefika nchini Afrika Kusini.


Wachezaji wa Leopards wapo jijini Oman tangu Januari 3 kwa maandalizi ya michuano ya mataifa ya Afrika yanato taraji kuzinduliwa Januari 19 nchini Afrika Kusini ambapo wanataraji kuelekea nchini humo siku tatu zijazo. Mechi yao ya kwanza watakutana na Ghana Januari 20, ya pili watakuwa na Niger Januari 24 na Mali tarehe 28 katika kundi B.
Waziri huyo amesema DRCongo inawania kuandaa michuano hiyo ya kombe la mataifa barani Afrika mwaka 2019, hivo timu ya taifa ya Congo haikwenda Afrika Kusini kufanya utalii
waziri Banza amewataka wachezaji kufanya vema kwenye michuano hiyo baada ya kukosekana kwa kipindi cha mika 6.
Mbali na hayo maandalizi yamekamilika takriban kwa asilimia kubwa kwa timu zote zilizo jumuishwa kwa makundi.

Wakati kamati ya maandalizi ya michuano ya kombe la mataifa huko Afrika kusini ikikosolew vikali na wadau wa soka Barani Afrika, shirikisho la soka barani Afrika limeipongeza viongozi wa Afrika kusini katika juhudi zao za kupokea michuano hiyo.

Kamati hiyo ya maandalizi inakosolewa vikali kwa uwepo wa uzembe katika shughuli za kuuza ticketi pamoja pia na kampeni za masoko. Juma lilopita ilivumbuliwa kuwa takriban tiketi laki tatu pekee dhidi ya laki tano ndizo ambazo tayari zimeuzwa.

Uongozi wa kamati hiyo umesema ticketi zote za mechi ya ufunguzi na ile ya mwisho tayari zimeuzikana zote, ambapo mechi ya uzinduzi itazipambanisha wenyeji wa michuano hiyo Bafana Bafana na Cape Verde.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire