lundi 14 janvier 2013

Lionel Messi awa mchezaji Bora kwa Mwaka 2012

     
Mwanasoka bora duniani kwa mwaka 2012, Leonel Messi
Mwanasoka bora duniani kwa mwaka 2012, Leonel Messi
REUTERS/Michael Buholzer

Na Lizzy Anneth Masinga
Lionel Messi mshambulizi wa Kimataifa wa Argentina anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya Barcelona nchini Uhispania kwa mwaka wa nne mfululizo ametajwa kuwa mchezaji bora duniani mwaka 2012 .

Messi alipigiwa kura na makocha na wapenzi wa soka duniani kutokana na umaahiri wake wa kufunga mabao katika klabu yake huku mwaka uliopita akifunga mabao 91 na pia kutajwa kuvunja rekodi ya miaka 40 iliyowekwa na Mjerumani Gerd Mueller kwa kufunga idadi kubwa ya mabao kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Messi mwenye umri wa miaka 25 hata hivyo amesema msimu uliopita haukuwa mzuri sana kwake kwa kile anachokieleza kuwa hakuisaidia klabu yake ipasavyo kushinda mataji mengi kama alivyotarajia.

Katika historia ya tuzo hiyo ni Lionel Messi na rais wa sasa wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini ndio ambao wameshinda taji hilo mara nne mfululizo.
Wachezaji wengine waliokuwa wanasaka taji hilo ni pamoja na Christiano Ronaldo anayechezea Real Madriid ambaye siku zote amekuwa akipambana na Messi bila ya mafanikio.

Andres Iniesta ambaye anacheza na Messi katika klabu ya Barcelona pia aliorodheshwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa wanatafuta taji hilo.Makocha wa timu mbalimbali pamoja na wachambuzi wa soka wanasema kuwa huu ni wakati wa Lionel Messi na huenda atashinda hadi mataji sita yajayo ikiwa ataendelea kuifungia klabu yake mabao kama anavyofanya sasa.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire