mardi 22 janvier 2013

Mali yapata ushindi dhidi ya Niger wakati DR Congo na Ghana wakitoka sare ya 2-2, leo ni zamu ya mabingwa watetezi Zambia

     
Saydou Keita mshambuliaji wa Mali akishangilia goli alilofunga dhidi ya Niger
Saydou Keita mshambuliaji wa Mali akishangilia goli alilofunga dhidi ya Niger
Reuters

Na Emmanuel Richard Makundi
Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC jana ilifanikiwa kupata sare ya magoli 2-2 dhidi ya timu ya taifa ya Ghana The Black Stars kwenye mchezo ambao Ghana walianza kwa kuongoza.

Wa kwanza kupata bao walikuwa ni vijana wa Ghana ambao waliandika bao lao la kwanza katika dakika ya 40 likifungwa na Emmanuel Agyemang Badu kabla ya dakika ya 49 Asamoah Gyan kuandika bao la pili na lakuongoza.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi amnapo DRC walianza kwa kulisakama lango la Ghana na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 53 likifungwa na Tresor Mputu kabla ya dakika ya 69 DRC kuzawadiwa Penalt iliyofungwa na Dieumerci Mbokani na kufanya matokeo kuwa sare ya mabao 2-2.
Katika mchezo wa pili timu ya taifa ya Mali walikuwa na kibarua dhidi ya Niger katika mchezo ambao Mali walifanikiwa kuchomoza na uchindi wa bao 1-0 lililofungwa na Saydou Keita.

Hii leo mabingwa watetezi timu ya taifa ya Zambia "Chipolopolo" watakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Ethiopia katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu kwa mabingwa hao watetezi.
Mchezo mwingine utazikutanisha timu ya taifa ya Nigeria "The Super Eagles" watakao kuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Burkina faso katika mchezo mwingine ambao unatarajiwa kuwa wakusisimua.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire