mardi 22 janvier 2013

Mabingwa watetezi Zambia walazimishwa sare na Ethiopia, wakati Nigeria nayo ikishindwa kutamba mbele ya Burikina Faso

     
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Zambia, Collins Mbesuma akifunga bao la kuongoza dhidi ya Ethiopia kwenye mchezo uliopigwa siku ya Jumatatu
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Zambia, Collins Mbesuma akifunga bao la kuongoza dhidi ya Ethiopia kwenye mchezo uliopigwa siku ya Jumatatu
Reuters

Na Emmanuel Richard Makundi
Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya Zambia jana ilishindwa kuanza vema michuano ya mwaka huu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ethiopia.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa upinzani kwa muda wote wa dakika 90, ulishuhudia Ethiopia wakikosa penalti katika kipindi cha kwanza kabla ya Zambia kuzinduka na kupata bao la kuongoza kupitia kwa Collins Mbesuma.
Mbesuma ambaye amerejeshwa kwenye kikosi cha mwaka huu baada ya kutoitwa kwenye mashindano ya mwaka jana, alionesha ni kwanini alistahili kuwepo kwenye michuano ya mwaka huu kwa kuiandikia bao la kuongoza timu yake.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo walikuwa ni Ethiopia ambao walipata bahati ya kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Adane Girma aliyeingia kwenye kipindi cha pili na kufanya mchezo umalizike kwa sare ya bao 1-1.
Katika mchezo mwingine, timu ya taifa ya Nigeria ilikuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Burkina Faso kwenye mchezo ambao umeshuhudia timu hizo zikitoka sare ya bao 1-1.
Alikuwa ni Emmanuel Emenike ndie aliyeanza kuiandikia bao la kuongoza Super Eagles kabla ya Alain Traore kuisawzishia timu yake na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Hii leo timu ya taifa ya Ivory Coast itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Togo, wakati miamba ya kaskazini timu ya taifa ya Algeria itakutana na wapinzani wao timu ya taifa ya Tunisia kwenye mchezo mwingine wa kundi D ambalo linatajwa kuwa ni kundi la Kifo.
tags: Burkina Faso - Ethiopia - Nigeria - Zambia

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire