vendredi 18 janvier 2013

Serikali ya DRC yakataa Madai ya M23 ya uundwaji wa Serikali ya mpito


Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila
Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila

Na Lizzy Anneth Masinga
Mazunguzo ya Kundi la Waasi wa M23 na Viongozi wa Serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC yanaendelea nchini Uganda lakini Serikali imekataa pendekezo la Waasi la kutaka iundwe Serikali ya Mpito.

Moja wapo ya madai ya waasi hao ni kutengeneza Serikali ya Mpito na Serikali ya Joseph Kabila huku mabadiliko mengine yakifanywa.
Akiongea na wanahabari Naibu Mwenyekiti wa wa ujumbe wa Serikali ya Kinshasa Padri Malumalu Mholongo kuhusu madai hayo amesema kuwa hakutakuwa na Serikali ya mpito kwa kuwa walishaachana na hatua hiyo tangu Mara ya mwisho kulipokuwa na Serikali ya mpito Mwaka 2003 mpaka Mwaka 2006.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa hakutakuwa na Serikali itakayoondoka kwa njia ya Silaha kupisha Serikali ya mpito na kuongeza kuwa watasikiliza Madai ya M23 lakini hawatashurutishwa kuyakubali.

Naye Msemaji wa M23 Betrand Bisimwa amesema wako tayari kuona utulivu unarejea Mashariki mwa Dr Congo na kuiomba Serikali kujitolea kwa vyovyote vile.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire