lundi 14 janvier 2013

Nyumba 40 zachomwa moto, wanawake sita wabakwa mashariki mwa DRC


Kutoka kushoto ni rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda Yoweri Museveni na rais wa DRC Joseph Kabila wakati walipokutana
Reuters
 

Na Victor Robert Wile
Mashirika ya kiraia huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesema kuwa Zaidi ya Nyumba 40 zimechomwa moto na wanawake 6 kubakwa.
Pia kumekuwa na matukio ya watu kuchukuliwa na kupelekwa katika maeneo yasiyojulikana huko mashariki mwa nchi hiyo baada ya kundi la watu wasiopungua 11 ambao mpaka sasa hawajulikani kutoka kundi gani,wakiwa na silaha kuvamia vijiji vya Kiravo,Makuta no na Kakwavia katika sekta ya Beni-Mbau.

Akizungumza kutoka jijini Goma msemaji wa Muungano wa Mashirika ya Kiraia akiwa pia naibu mwenyekiti wa muungano huo,Omari Kavota amethibitisha tukio hilo na kaongeza kwamba waasi wa ADF-NALU wa Uganda wamezidisha vitendo vya utekaji nyara huku serikali ikisalia kimya.
Kufuatia hali hiyo kuendelea kushuhudiwa mara kwa mara katika eneo hilo, muungano wa mashirika ya kiraia umewatolea wito wabunge pamoja na waziri wa ulinzi ambae pia anahusika na mambo ya ndani kueleza nini matunda ya operesheni nyingi za kijeshi zilizoratibiwa katika eneo hilo, huku mauaji na vitendo vya ukatili vikiendelea kuripotiwa namna hiyo.

Mazungumzo ya kusaka suluhu huko Mashariki mwa DR Congo kati ya Serikali ya kinshasa na waasi wa m23 yataendelea bila tatizo huko kampala uganda hata baada ya UN kutishia kuweka vikwazo.

Mwenyekiti wa mazungumzo hayo Chrispus Kiyonga amethibitisha kuwa mazungumzo hayo yataendelea kwa kuzishirikisha pande mbili za Serikali na waasi wa M23.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire