mardi 1 janvier 2013

Watu 60 wapoteza maisha nchini Cote D'Ivoire wakati wa sherehe za kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013

     
Mabaki ya nguo na viatu vya wananchi wa Cote D'Ivoire waliopoteza maisha kwenye sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2013
Mabaki ya nguo na viatu vya wananchi wa Cote D'Ivoire waliopoteza maisha kwenye sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2013

Na Nurdin Selemani Ramadhani

Watu wanaokadiriwa kufikia sitini wamepoteza maisha nchini Cote D'Ivoire na wengine zaidi ya mia mbili wamejeruhiwa wakiwa kwenye sherehe za kuukaribishwa mwaka mpya kwenye uwanja wa mpira wa miguu Jijini Abidjan. Vifo na majeruhi hayo yamesababishwa na ghasia ambazo zilizuka na kuchangia watu kukimbia ovyo wakati ambapo mafataki yakiwa yanapigwa kama sehemu ya shamra shamra za kuukaribishwa mwaka 2013.
Mkuu wa Jeshi kwenye Kikosi cha Upkozi Luteni Kanali Issa Sako amethibititsha kutokea kwa vifo na majeruhi hayo kwenye Televisheni ya Taifa na kusema vilichangiwa na mafataki ambayo yalikuwa yanapigwa kuukaribisha mwaka mpya.
Luteni Kanali Sako amesema watu hao wakiwa kwenye shamra shamra hizo za kuikaribishwa mwaka 2013 ndipo kulipotokea kukanyagana na watu waliojumuika usiku huo kupoteza maisha.

Sako amesema idadi ya wale ambao wamepoteza maisha pamoja na majeruhi iliyotolewa ni ya awali na kwa sasa wanaendelea kusaka idadi rasmi kujua watu ambao wamefikwa na umauti pamoja na majeruhi.
Luteni Kanali Sako ameongeza sababu za awali ambazo zimetajwa kuchangia vifo vya watu hao ni kukosa hewa ya kutosha kutokana na msongamano pamoja na kukanyagana kulikozuka kwenye umati huo.
Wengi ambao walipoteza maisha walikuwa wanagombea kutoka nje ya Uwanja huo baada ya kuonekana kuzidiwa kwa hali ya joto na ndipo idadi kubwa ya watu iliposhindwa kutoka kwa wakati wengine wakaanza kukanyangwa.

Picha ambazo zimeoneshwa na Televisheni ya Taifa ya Cote D'Ivoire RTI zimeonesha miili ya watu ikiwa chini baada ya kupoteza uahai huku vitu kama nguo na viatu vikiwa vimezagaa kwenye eneo la mlango wa kutoka Uwanja uliokuwa unatumika kusherehekea mwaka mpya.
tags: Côte d’Ivoire

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire