vifaru vya monusco nchini DRCongo
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRCongo
(MONUSCO) sasa wameingilia kati kulisaidia jeshi la FARDC kupambana na
waasi wa kundi la M23 ambao wameanzisha vita tangu juzi, na watu sita
wanaripotiwa kupoteza maisha baada ya waasi kurusha makombora
yalioangukia kwenye maeneo wanakoeshi raia wengi mjini Goma.
Msemaji wa Monusco luteni kanali Prosper Basse amesema kwa sasa
wanathibitisha kuwa vikosi vya Umoja wa Mataifa vinapambana sanjari na
jeshi la FARDC kupambana na waasi katika kuwalinda raia wa mji wa kibati
lakini pia jiji la Goma. Hatuwa hiyo amesema msemaji huto wa Monusco
imechukuliwa baada ya mashambulizi yaliotokea jana katika viounga vya
jiji la Goma na kusababisha vifo vya watu wanne.
Luteni Kanali Bass amesema MONUSCO imechukua mipango yote sahihi kwa ajili ya kutowa uwezo zaidi kwa kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa nchini humo kupambana na waasi wa M23 sanjari na jeshi la FARDC. Amesisitiza kuwa hii ndio hatuwa muafaka ya kuwalinda raia na mali zao.
Kulingana na duru za kijeshi ya Magharibi, Afrika Kusini iliowatuma wanajeshi wake kujiunga na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa wameshambulia kifaru cha kijeshi T 55 kilichokuwa kinatumiwa na kundi la waasi wa M23 ambacho kilikuwa kimepiga kambi katika mji wa kibati. Taarifa ambayo imekanushwa na wizara ya ulinzi ya Afrika Kusini.
Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini Siphiwe Dlamini amesema chanzo hicho sio sahihi, ni kweli kwamba majeshi ya Umoja wa Mataifa yapo karibu na eneo hilo na muda wowote wakishambuliwa watajibu mapigo.
Wakati hayo yanajiri, waziri wa habari ambaye pia ni msemaji wa serikali ya DRCongo Lambert Mende amewaambia waandishi wa habari katika mkutano wake kwamba bomu zilizo rushwa na kuanguka jijini Goma zilizo sababisha vifo vya watu 4, zilirushwa kutoka upande wa Rwanda katika vijiji vya Mukamira na Rugero Wilaya ya Rubavu.
Membe amesema katika mapigano hayo yalioanza tangu siku ya Jumatano waasi 17 wameuawa huku wengine 12 wakitekwa.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire