lundi 4 mars 2013

Kenya yatakiwa uchaguzi wa amani kudhidirisha ukomavu wa demokrasia

 
KENYA-MAREKANI - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 02 machi 2013 - Taarifa za ivi karibuni : Jumamosi 02 machi 2013 
Wagombea wa uraisi nchini Kenya
Wagombea wa uraisi nchini Kenya
rfi

Na Martha Saranga Amini

Wakati harakati za kampeni za uchaguzi wa uraisi zinafikia ukingoni nchini Kenya, Marekani imewataka raia wa Kenya kufanya uchaguzi wa amani ili kumpata kiongozi mpya kwa amani.

Akizungumza kwa niaba ya serikali naibu msemaji wa serikali ya Marekani Patrick Ventrell ameongeza kuwa Kenya inapita katika kipindi cha muhimu na kihistoria na hivyo kuwasihi wagombea kuhakikisha wanaepuka kuwa sababisho la umwagaji damu kama uliowahi kutokea katika uchaguzi wa mwaka 2007.
Hata hivyo hali ya mvutano imeongezeka ambapo serikali ya Marekani imewataka wakenya kutumia fursa hiyo kudumisha ukomavu wa demokrasia na kutekeleza matakwa ya katiba mpya.
Msemaji huyo amesema kuwa ni matarajio ya wengi kuwa wakenya hawatajali jinsi,kabila,dini,eneo analotoka mgombea ili kuchagua bali bali watamchagua kiongozi bora kulingana na sifa stahiki.
Takribani raia elfu moja walipoteza maisha huku laki sita wakiyakimbia makazi yao katika machafuko yaliyotokea katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2007.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire