vendredi 23 août 2013

Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRCongo sanjari na wanajeshi wa FARDC kupambana na waasi wa M23 wanaotishia usalama

vifaru vya monusco nchini DRCongo
vifaru vya monusco nchini DRCongo

Na Ali Bilali
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRCongo (MONUSCO) sasa wameingilia kati kulisaidia jeshi la FARDC kupambana na waasi wa kundi la M23 ambao wameanzisha vita tangu juzi, na watu sita wanaripotiwa kupoteza maisha baada ya waasi kurusha makombora yalioangukia kwenye maeneo wanakoeshi raia wengi mjini Goma.

Msemaji wa Monusco luteni kanali Prosper Basse amesema kwa sasa wanathibitisha kuwa vikosi vya Umoja wa Mataifa vinapambana sanjari na jeshi la FARDC kupambana na waasi katika kuwalinda raia wa mji wa kibati lakini pia jiji la Goma. Hatuwa hiyo amesema msemaji huto wa Monusco imechukuliwa baada ya mashambulizi yaliotokea jana katika viounga vya jiji la Goma na kusababisha vifo vya watu wanne.

Luteni Kanali Bass amesema MONUSCO imechukua mipango yote sahihi kwa ajili ya kutowa uwezo zaidi kwa kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa nchini humo kupambana na waasi wa M23 sanjari na jeshi la FARDC. Amesisitiza kuwa hii ndio hatuwa muafaka ya kuwalinda raia na mali zao.

Kulingana na duru za kijeshi ya Magharibi, Afrika Kusini iliowatuma wanajeshi wake kujiunga na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa wameshambulia kifaru cha kijeshi T 55 kilichokuwa kinatumiwa na kundi la waasi wa M23 ambacho kilikuwa kimepiga kambi katika mji wa kibati. Taarifa ambayo imekanushwa na wizara ya ulinzi ya Afrika Kusini.

Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini Siphiwe Dlamini amesema chanzo hicho sio sahihi, ni kweli kwamba majeshi ya Umoja wa Mataifa yapo karibu na eneo hilo na muda wowote wakishambuliwa watajibu mapigo.

Wakati hayo yanajiri, waziri wa habari ambaye pia ni msemaji wa serikali ya DRCongo Lambert Mende amewaambia waandishi wa habari katika mkutano wake kwamba bomu zilizo rushwa na kuanguka jijini Goma zilizo sababisha vifo vya watu 4, zilirushwa kutoka upande wa Rwanda katika vijiji vya Mukamira na Rugero Wilaya ya Rubavu.

Membe amesema katika mapigano hayo yalioanza tangu siku ya Jumatano waasi 17 wameuawa huku wengine 12 wakitekwa.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire