Waasi wa M23 wanaotakiwa kuondoka mjini Goma licha ya baadhi kuendelea kuonekana mjini humo.
RFIWapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 ambao walikuwa wanaushikilia Mji wa Goma wameanza kuondoka katika eneo hilo kutekeleza amri ya Viongozi wa Ukanda wa Maziwa Makuu uliowataka kuweka silaha chini na kuondoka mara moja.
Msemaji wa Kundi la M23 Kanali Vianney Kazarama amesema wapiganaji wao wote watakuwa wameondoka katika Mji wa Goma ifikapo siku ya Ijumaa kutekeleza makubaliano yao na serikali.
Waziri wa Habari na Mawasiliano wa serikali ya Kinshasa ambaye pia ni msemaji wa serikali Lambert Mende Omulanga ametaka M23 kuondoka licha ya kuweka bayana wamekuwa hawawaamini pale wanapotakiwa kutekeleza amri zilizotolewa.
Hofu na wasiwasi ungali umetanda miongoni mwa wananchi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kipindi hiki ambacho taarifa zikisema Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 wameanza kuondoka katika Mji wa Goma waliokuwa wanaushikilia.
Hali hiyo imekuja kipindi hiki ambacho baadhi ya Wapiganaji wa Kundi la M23 wakiendelea kuonekana katikja mitaa ya Mji wa Goma licha ya wenyewe kutangaza kuondoka.
Kwa upande wake Msemaji wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa Vinavyolinda Amani nchini DRC maarufu kama MONUSCO Manodje Mounoubai ameshindwa kuthibitisha kama kweli wapiganaji wa M23 wameondoka Goma.
Marekani kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje Hillary Clinton ametaka Jumuiya ya Kimataifa kuungana kuisaidia serikali ya Kinshasa katika mapambano yao dhidi ya Kundi la Waasi la M23.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire