lundi 24 décembre 2012

Goma: Obama ainyooshea kidole cha lawama Rwanda dhidi ya machafuko yanayoendelea mashariki mwa DRC

Rais wa Marekani Barak Obama
REUTERS/Jason Reed

Na Flora Martin Mwano

Rais wa Marekani Barrack Hussein Obama amemtaka rais wa Rwanda Paul Kagame kuacha kuwasaidia waasi wa kundi la M23 wanaopambana na wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Rais Obama amempigia simu Rais Kagame na kumsisitizia umuhimu wa kusitisha msaada huo kwa waasi ambao anasema unaifanya Rwanda kuwa kikwazo kwa upatikanaji wa amani Mashariki mwa DRC na katika kanda ya Maziwa Makuu.

Hata hivyo Rwanda imeedelea kukanusha kuwawaunga mkono waasi hao wa M23 ambao kwa sasa wanajadiliana na serikali ya DRC kumaliza tofauti zao katika mazungumzo ya amani yanayoendelea jijini Kampala nchini Uganda.

Aidha Marekani imehimiza kukamakatwa kwa viongozi wa waasi Sylvestre Mudacumura na Bosco Ntaganda na kufikishwa katika Mahakama ya kimatifa ya uhalifu wa kivita ICC kwa tuhuma za kuhusika na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
tags: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - Marekani - Rwanda

1 commentaire:

  1. OBAMA ni kwa nini humu chape au kumufuatisha mwenziye Kadafi huyo mujanja na muwaji Kagamé

    RépondreSupprimer