lundi 24 décembre 2012

RDC: Naibu mwenyekiti wa polisi auawa Mkoani Kivu Kaskazini


Polisi mashariki mwa DRCongo
Polisi mashariki mwa DRCongo

Na Ali Bilali

Naibu mkuu wa Polisi katika Jimbo la Kivu ya Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC Meja Bertin Chirumana, ameuwawa kwa kupigwa risasi na kundi la watu wasiojulikana bado katika mjini Goma.

Meja Bertin Chirumana amepigwa risasi na kufa papo hapo mjini Goma mwishoni mwa juma lilopita. Uchunguzi umeanzishwa ili kubaini wahusika wa tukio hilo la mauaji.

Duru kutoka katika eneo hilo zaarifu kuwa matukio kama hayo ya mauaji ya kuvizia yamekuwa yakishuhudiwa wakati wa jioni mjini Goma na kutekelezwa na kundi la watu wasiojulikana.

Hatua ya waasi wa kundi la M23 kuuteka mji wa Goma mwezi uliopita, ilipelekea watu elfu moja na mia tano (1500) waliokuwa gerezani mjini Goma walitoroka na wengine kukimbilia maeneo yasiyojulika bado hadi sasa.
Hata hivyo waasi wa kundi la M23 baada ya kuondoka mjini Goma kufuatia azimio la viongozi wa nchi za ukanda wa maziwa makuu na shinikizo la Jamii ya Kimataifa, na sasa wanapatikana kwenye umbali wa kilomita ishirini na mji huo wa Goma, ili kupisha mazungumzo na serikali ya Kinshasa yanayoendelea mjini Kampala.
tags: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire