Katika hatua nyingine Maelfu ya wafuasi wa rais wa zamani wa Misri Mohammed Morsi wamekusanyika jijini Cairo kushinikiza kurejeshwa madarakani kwa kiongozi wao aliyepiunduliwa na jeshi siku ya Jumatano.
Jeshi nchini humo limesema kuwa litaruhusu maandamano ya mani nchini humo wakati huu rais wa mpito Adly Mahmud Mansour, akisema kuwa uchaguzi Mkuu utafanyika hivi karibuni ili kuwapa nafasi wananchi wa Misri kuamua ni nani wanayetaka awaongoze.
Chama cha Muslim Brotherhood kimeitisha Maandamano hayo kupinga mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa dhidi ya Kiongozi wa Chama chao, na kuwataka Raia kushiriki hii leo baada ya Swala ya Ijumaa
Jeshi limeapa kuwashugulikia watu watakaoandamana na kuleta vurugu na kuongeza kuwa maandamano hayo yanapaswa kuwa ya amani na si vinginevyo.
Jeshi la Misri limechapisha taarifa yake kwenye ukurasa wa Facebook likieleza kuwa watu wengi walijeruhiwa katika makabiliano baina ya wafuasi wa Morsi na upande uliokua ukimpinga huko Nile Delta kabla ya kufanyika kwa maandamano ya leo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire