samedi 27 juillet 2013

Umoja wa Mataifa UN wakemea ushirikishwaji wa watoto kwenye mapigano Mashariki mwa DRC

Unicef

Na Flora Martin Mwano
Umoja wa Mataifa UN kupitia kwa shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF umetoa wito kwa pande zinazokinzana nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuheshimu sheria za kimataifa kwa kuwaachia huru watoto wote wanaoshirikishwa kwenye makundi ya wapiganaji katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF, watoto zaidi ya elfu mbili wamekuwa wakitumiwa kama wapiganaji katika mapigano ya yanayoendelea hivi sasa kati ya vikosi vya serikali na waasi wa kundi la M23.

Balozi wa UNICEF Barbara Bentein amesema wana uthibitisho wa watoto walio chini ya miaka umri wa kumi na minane kutumiwa kama wapiganaji, wakati wengine kadhaa wamekuwa wakiuawa na kujeruhiwa.

Wito wa UNICEF unafuatia ule wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ambaye ameitaka Serikali ya Kinshasa na waasi wa M23 kurejea kwenye meza ya mazungumzo huko Kampala ili kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Mapigano baina ya vikosi vya serikali na M23 yaliyozuka tena mwezi huu yameendelea kuhatarisha usalama wa mashariki mwa DRC hatua iliyosababisha watu zaidi ya elfu tano kuyahama makazi yao na baadhi kukimbilia katika nchi jirani.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire