mardi 2 juillet 2013

Waziri wa mambo ya nje wa Misri ajiuzulu

Waziri wa mambo ya kigeni wa Misri Mohammed Kamel
Waziri wa mambo ya kigeni wa Misri Mohammed Kamel
shorouknews.com

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Misri Mohammed Kamel amejiuzulu nafasi yake leo Jumanne akiwa ni kiongozi wajuu kuchukua uamuzi huo muda mfupi baada ya mawaziri wengine wanne kujiuzulu hapo jana,Shirika la habari la Taifa hilo MENA limearifu.

Hatua ya waziri huyo kujiuzulu imezidi kuiyumbisha serikali ya rais Mohamed Morsi ambaye ameonywa na jeshi kuwasikiliza wananchi ambao wamempa saa 48 kutatua mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo ama sivyo jeshi litaingilia kati.

Hata hivyo ofisi ya rais nchini Misri imekataa kutekeleza matakwa ya Jeshi na kusema kuwa itaendelea na mipango yake ya kulipatanisha taifa hilo.

Taarifa ya Ofisi ya Rais imekemea hatua ya jeshi kutaka kuingilia kati na kudai kuwa hatua ya jeshi hilo italeta mgawanyiko zaidi na kutishia kuvunjika kwa amani.

Watu wanaomuunga mkono Rais Morsi ndani ya Chama cha muslim Brotherhood wamesema kuwa kitendo cha kumtetea Morsi ni kutetea uhalali wa rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire