jeudi 18 juillet 2013

Dunia inaadhimisha siku ya kuzaliwa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela huku mwenyewe akisalia hospitali kwa matibabu

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela wakati akizungumza kwenye moja ya ziara zake
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela wakati akizungumza kwenye moja ya ziara zake
Reuters

Na Emmanuel Richard Makundi
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela hii leo anasherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini huku familia yake ikisema afya ya kiongozi huyo inaimarika.
Mtoto wa kiongozi huyo Zindzi Mandelea amewaambia wanahabari mjini Johanesberg kuwa afya ya baba yake inaendelea kuimarika na huenda akareuhusiwa wakati wowote.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya Afrika Kusini inasema kuwa madaktari wanaomtibu mzee Mandela wamdhibitisha kuwa afya ya kiongozi huyo inaendelea vizuri na huenda akaruhusiwa kutoka hospitali.
Taarifa kuhusu afya ya Mandela zinatolewa wakati huu ambapo taifa hilo hii leo linafanya sherehe ya kukumbuka kuzaliwa kwa kiongozi huyo anaetimiza miaka 95 hii leo.

Mbali na wananchi wa Afrika Kusini ambao hii leo wanasherehekea siku hiyo, dunia pia inaadhimisha siku hii ambayo inatambuliwa pia na Umoja wa Mataifa kama siku ya Mandela 'Mandela Day'.

Mzee Mandela anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini ambako amelazwa kwa zaidi ya mwezi mmoja hivi sasa kutokana na kusumbuliwa na maradhi ini.
Viongozi mbalimbali wa kidini nchini Afrika Kusini wametoa wito kwa wananchi kumuombea kiongozi huyo ili aweze kurejea kwenye hali yake ya kawaida.

Dunia inaadhimisha siku hii kwa wananchi kushiriki shughuli za kijamii kwa dakika sitini na saba, huku rais Jackob Zuma akisherekea siku hii kwa kendesha harambee ya kuchangia mfuko wa Nelson Mandela.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire