dimanche 28 juillet 2013

Papa Francis awaunga mkono vijana wanaodai mabadiliko ya jamii

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis akiwa Rio De Jeneiro,Brazili
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis akiwa Rio De Jeneiro,Brazili
REUTERS/Ueslei Marcelino

Na Martha Saranga Amini

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amewaunga mkono vijana waliochukua hatua ya kuandamana kwa lengo la kutaka mabadiliko akihutubia takribani watu milioni mbili huko Brazil.

Papa Francis aliwaambia waumini wa kanisa Wakatoliki ambao wengi wao walikuwa vijana waliokusanyika katika pwani moja huko Rio de Janeiro kwamba alifuatilia habari duniani na kuona wimbi kubwa la vijana likifanya maandamano kwa lengo la kueleza uhitaji wa haki na udugu.
Papa aliongeza kuwa Vijana wanaoonekana wakiandamana wameamua kuwa watendaji wa mabadiliko na kuwataka vijana kuwajibika wanapoguswa na masuala ya kijamii na kisiasa katika maeneo mbalimbali duniani.
Mamilioni ya waandamanaji walijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini brazil mwezi uliopita wakipinga ufisadi,matumizi mabaya ya mali ya umma,na gharama kubwa za kufanyika kwa kombe la dunia mwaka 2014 nchini humo maandamano ambayo mara zote huishia kuwa ghasia.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire