mardi 2 juillet 2013

Obama asikitishwa na hali ya usalama DRC

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama
politico.com

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Rais wa Marekani Baraka Obama akiwa ziarani nchini Tanzania amesema kuwa viongozi wa Afrika wanawajibika kubeba jukumu la kukabiliana na migogoro mbalimbali inayolikabili bara hilo ukiwemo mgogoro wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

STORY BARAKA OBAMA DRC WRAP PAD
02/07/2013
Rais Obama amesema kuwa wananchi wa DRC wana haki ya kuishi kwa amani na hivyo kuepuka mtatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Rais Obama amesema kuwa Marekani ipo tayari kushirikiana na Umoja wa Mataifa na wadau wengine kushughulikia mgogoro wa DRC na kusifu juhundi za Tanzania za kulinda amani katika kanda ya maziwa makuu.

Akizungumzia suala la Zimbabwe Obama amesema wananchi wa Zimbabwe ni vema wakalindwa dhidi ya vitisho vya utawala usio wa kidemokrasia huku akitoa wito wa kufanyika uchaguzi ulio huru na wa haki.

Katika hatua nyingine Obama ameelezea umuhimu wa bara la Afrika kujenga misingi ya utawala wa kidemokrasia ambao utasaidia kuwa na serikali zinazowajibika kwa raia wake.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire