vendredi 6 septembre 2013

Mvutano wa Rwanda na Tanzania waingia katika sura mpya baada ya Rais Kikwete na Kagame kukutana

DRCONGO-TANZANIA-RWANDA-UGANDA - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Ijumaa 06 septemba 2013 - Taarifa za ivi karibuni : Ijumaa 06 septemba 2013


Rais Kikwete na Rais Kagame
RFI

Na Victor Robert Wile
Viongozi wa Rwanda na Tanzania wametuma ujumbe kwa dunia kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana licha ya kuripotiwa kuwepo tofauti baina pande hizo mbili wakati huu majeshi ya DRC yakionyesha kusita kusimamisha mapigano ili kurejea katika meza ya mazungumzo  na waasi wa M23.

Kukutana kwa viongozi wa Tanzania na Rwanda huenda kukaondoa wingu lililokua limetanda huku dalili za mgogoro baina ya nchi hizo mbili hali iliyotakana pamoja na mambo mengine uliibuka baada ya Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kutaka Rwanda na Uganda kuzungumza na waasi wake.

Rais Kikwete alitoa ushauri huo akilenga kuonyesha kuwa htua hiyo ingeweza kusaidia kumalizika kwa mgogoro unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Marais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda wamekutana jijini Kampala nchini Uganda kando ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya nchi zaMaziwaMakuu.
Viongozi wa Maziwa Maku walikuwa wakijadili kuhusu mzozo unaendelea mashariki mwa DRCongo kati ya waasi wa wa Kundi la M23 na wanajeshi wa serikali ya DRCongo wa FARDC.
Kumekuwa na viashiria kuwepo na mzozo kati ya nchi hizo mbili baada ya kauli mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa huku na kule. 

Kukutana kwa viongozi hawa wawili kunaleta matumaini kwamba watamaliza tofauti zao. Wachambuzi wa maswala ya siasa wanaona kwamba hiyo ni hatuwa muhimu sana.


Viongozi wa Jumuiya ya nchi za ukanda wa maziwa makuu katika kikao cha cha dharura hapo jana jijini Kampala Uganda, wametowa siku tatu kwa waasi wa M23 na serikali kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza mzozo huo.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire