lundi 30 septembre 2013

MONUSCO yaanza kuchunguza mauaji ya waandamanaji Goma


DRCONGO-MONUSCO - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumatatu 26 agosti 2013 - Taarifa za ivi karibuni : Jumatatu 26 agosti 2013

Wanajeshi wa MONUSCO

Na Victor Melkizedeck Abuso
Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa Mashariki kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MUNUSCO, linasema  limeanza kuchunguza madai dhidi ya vikosi vyake kutekeleza mauaji ya watu wawili mjini Goma mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kiongozi wa MONUSCO Martin Kobler, amesema kuwa jeshi hilo likishirikiana na lile la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FRDC wameanzisha uchunguzi huo kubaini ukweli kuhusu mkasa huo.
Walioshuhudia mauaji hayo wanasema wanajeshi wa MONUSCO raia wa Uruguay waliwapiga risasi watu wawili wakati walipokuwa wanasambaratisha kundi la waandamanaji lililokuwa limevamia kambi ya jeshi hilo.
Mauaji haya yametokea siku moja tu baada ya kutokea kwa shambulizi la bomu  mjini Goma na kusabisha vifo vya watu watatu na pia kuwajeruhiwa wanajeshi watatu wa kulinda amani.
Wiki iliyopita, waasi wa M 23 na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamekuwa wakipambana karibu na mji wa Goma huku kila upande ukituhumiana kuanzisha makabiliano hayo.
Ukosefu wa amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeilazimu serikali ya Uingereza kuwaagiza  raia wake wote wanaoishi na kufanya kazi mjini Goma kuondoka kwa kuhofia usalama wao.
Kiongozi wa kundi la M 23 Betrand Bissimwa amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akilalamikia kuhusika kwa jeshi la kulinda amani katika mzozo wa Mashariki mwa nchi hiyo na kutekeleza mauaji .
Jeshi la serikali kwa upande wake linasema kuwa litaendelea kulinda mipaka ya nchi hiyo na pia kukabiliana na makundi ya waasi likiwemo la M 23 ikiwa litaanza kuwavamia.
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Kinsasha na waasi wa M 23 yamegonga mwamba jijini Kampala Uganda suala ambalo limeendelea kuhatarisha usalama Mashariki mwa nchi hiyo.
Mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umekuwa ukiendelea kwa kipindi kirefu na ulizorota mwaka uliopita baada ya kuzuka kwa kundi la M23 lililodai kubaguliwa na serikali ya Kinsasha.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikituhumiwa na jirani zao DRC na Umoja wa Mataifa kufadhili na kuwaunga mkono waasi wa M 23 tuhma ambazo Kigali imeendelea kukanusha.
Jeshi la kulinda la umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini tayari liko Mashariki mwa nchi hiyo kukabiliana na makundi ya waasi.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire