lundi 30 septembre 2013

Mapigano yazuka tena huko mashariki mwa DRCongo baina ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali vya FARDC

DRCongo-mapigano - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Thursday 22 agosti 2013 - Taarifa za ivi karibuni : Thursday 22 agosti 2013

Wanajeshi wa serikali ya Congo FARDC Julay 22 huko Kibati.
Wanajeshi wa serikali ya Congo FARDC Julay 22 huko Kibati.
REUTERS/Kenny Katombe

Na Ali Bilali
Mapambano makali yanaripotiwa tangu jana na leo baina ya waasi wa kundi la M23 na majeshi ya DRCongo FARDC kaskazini mwa mji wa Goma mashariki mwa nchi hiyo, duru za kijeshi kutoka katika mkoa wa Kivu ya kaskani zimethibitisha.

Kanali Olivier Hamuli msemaji wa FARDC kivu kaskazini mashariki mwa DRCongo azungumzia kuhusu mapigano na kundi la waasi wa M23 22 2013
 
22/08/2013
Mapigano hayo yalioanza jana jumanne jioni na kuendelea hadi leo alhamisi yanaripotiwa katika vijiji vya mutaho na Kibati kwenye umbali wa zaidi ya kilometa ishirini na jiji la Goma. Hakuna takwimu zozote ambazo zimetolewa kuhusiana na mapigano hayo.
Katika taarifa iliotolewa na kundi la waasi wa M23, kupitia msemaji wake Amani Kabasha, kundi hilo limelinyooshea kidole cha lawama jeshi la DRCongo FARDC kwa kuanzisha tena vita baada ya kushindwa juhudi za kidiplomasia wiki za hivi karibuni.
Kwa mujibu wa msemaji huyo wa M23, kuanzishwa tena kwa mapigano na jeshi la FARDC huko mashariki mwa DRCongo ni kuvunja mapendekezo ya viongozi wa kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, pamoja pia na pendekezo la kikao cha viongozi wa ukanda wa maziwa makuu na kile cha Jumuiya ya kiuchumi cha viongozi wa nchi za kusini mwa Afrika SADC, walioomba kurejea kwenye meza ya mazungumzo huko Kampala nchini Uganda.
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa jeshi la Congo ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema vikosi vya FARDC vilishambuliwa katika ngome zao vilivyokuwa vikikalia tangu mwezi uliopita kwenye umbali ta takriban kilometa ishirini na jiji la Goma. Hata hivo afisaa huyo hakutowa takwimu zozote kuhusu mapigano hayo.
Meja Modeste Bahati afisaa anaye husika na mawasiliano katika kundi la M23 amesema vikosi vya M23 vimebaki kwenye ngome zao, bila hata hivyo kutowa ufafanuzi zaidi.

Upande wake msemaji wa Jeshi la FARDC katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini Mashariki mwa DRCongo Kanali Olivier Hamuli amesema, jeshi la FARDC ni jeshi la taifa, ninafanya juhudi zote kuhakikisha linawalinda wananchi na mali zao.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire