mardi 10 septembre 2013

Mazungumzo kati ya M23 na Serikali ya Kinshasa yanatarajiwa kuanza hii leo mjini Kampala

M23-DRC-UGANDA - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumanne 10 septemba 2013 - Taarifa za ivi karibuni : Jumanne 10 septemba 2013

Renee Abandi, mkuu wa ujumbe wa M23 kwenye mazungumzo ya Kampala
Renee Abandi, mkuu wa ujumbe wa M23 kwenye mazungumzo ya Kampala
Reuters

Na Emmanuel Richard Makundi
Mazungumzo ya amani kati ya waasi wa M23 na upande wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC yanatarajiwa kuanza hii leo mjini Kampala, Uganda kusaka suluhu ya mzozo wa mashariki mwa nchi hiyo.

Mazungumzo haya ambayo yanakuwa ni ya pili kufanyika baada ya yale ya awali kuvunjia bila kupatikana suluhu, yanakuja kufuatia maazimio ya viongozi wa nchi 11 za maziwa makuu kutaka pande hizo mbili kurejea kwenye meza ya mazungumzo.
Tayari ujumbe wa M23 unaoongozwa na Renee Abandi umeshawasili mjini Kampala toka mwishoni mwa juma ukisisitiza utayari wake wa kumaliza machafuko mashariki mwa nchi hiyo.
Hapo jana mkuu wa kundi la M23, Betrand Bisimwa alitoa mashrti ya kundi lao kusalimisha silaha akidai kuwa watafanya hivyo iwapo kundi la FDLR litafurushwa nchini humo pamoja na wakimbizi wa kongo kurejea nyumbani.
Masharti haya ambayo yanaonekana ni mapya na yanayoweza kutekelezeka yanakuja wakati huu ambapo Serikali ya Kinshasa imeonesha wasiwasi wake kuhusu kusitisha vita dhidi ya kundi ikidai kuwa kutatoa mwanya wa kundi hilo kujipanga upya.
Mpaka sasa haijajulikana ni lini hasa mazungumzo haya yataanza kwakua ujumbe wa Serikali ya Kinshasa bado haujawasili mjini Kampala wala haijajulikana utaongozwa na nani.
tags: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - Kundi la Waasi la M23 - Uganda

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire