samedi 8 décembre 2012

Viongozi wa SADC kukutana jijini Dar es Salaam, Tanzania kujadili mgogoro wa DRC


Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Bernad Membe (katikati) akizungumza na waandishi kueleza maandalizi ya mkutano wa SADC mwishoni mwa juma hili
Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Bernad Membe (katikati) akizungumza na waandishi kueleza maandalizi ya mkutano wa SADC mwishoni mwa juma hili
RFI

Na Emmanuel Richard Makundi
Waasi wa kundi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC linatarajiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa Serikali ya DRC siku ya alhamisi na Ijumaa mjini Kampala Uganda

Mazungumzo hayo yanakuja ikiwa zimepita siku chache toka waasi hao waondokea kwenye mji wa Goma mashariki mwa nchi hiyo ambao walikuwa wanaushikilia.
Waziri wa ulinzi wa Uganda Richard Muyej Mangez amesema kuwa mazungumzo hayo yanaanza baada ya majeshi ya DRC kurejea kwenye mji wa Goma kama walivyokubaliana kwenye mkutano uliofanyika majuma kadhaa yaliyopita chini ya viongozi wa Jumuiya ya nchi za maziwa makuu ICGLR.
Miongoni mwa masuala ambayo yalikuwa yamekubaliwa kwenye mkutano uliopita ni pamoja na waasi wa M23 kuondoka kwenye mji wa Goma pamoja na Serikali kukubali kukaa meza moja na waasi hao kumaliza tofauti zao.
Serikali ya Kongo imesema madai ya M23 mengi hayawezi kutekelezeka kwasasa kwakuwa yalikwishatekelezwa kwenye mkataba ambao ulitiwa saini mwaka 2009 kati ya Serikali na makundi ya waasi nchini humo.
Viongozi wa waasi wa M23 wametishia kurejea kwenye mji wa Goma iwapo Serikali itashindwa kutekeleza madai yao wala kufanya mazungumzo nao jambo ambalo Serikali ya DRC kwasasa imesema itapambana.
Wakati huohuo mwishoni mwa juma viongozi wa jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC wanatarajiwa kukutana mjini Dar es Salaam Tanzania kujadili hali ya mambo nchini DRC pamoja na mgogoro kisiasa wa Madagascar.
Mkutano huo pia unatarajiwa kuhudhuriwa na rais wa Afrika Kusini Jackob Zuma.
Kwenye mkutano huo pia nchi ya Tanzania itawasilisha ripoti yake kuhusu maendeleo ya usuluhishi kwa nchi ya Madagascar kati ya viongozi wawili mahasimu rais Andy Rajoelina na yule aliyepinduliwa Marc Ravalomanana.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire