mardi 9 avril 2013

Kumbukumbu za mauaji ya Kimbare Rwanda

 8 Aprili, 2013 - Saa 07:46 GMT
Mmoja wa washukiwa wawakuu wa mauaji ya Kimbare Leon Mugesera
Wanyarwanda wanaanza wiki ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ikiwa ni miaka 19 sasa tangu yatokee.
Na katika juhudi za kuponya nchi, Rwanda imekua na nguzo za kuleta maridhiano pamoja na mfumo wa sheria kuwajibisha waliohusika.
Licha ya juhudi hizi bado waathirika wengi wangali kupona mafadhaiko kutokana na mauaji hayo na sasa juhudi zimeanza kuwanusuru raia dhidi ya matatizo ya kiwewe.
Mwaka huu wanyarwanda wanakumbuka siku hii kwa kauli mbiu ya ''Tukumbuke mauaji ya kimbare dhidi ya Watusti tukijitahidi kujenga nchi yetu.''
Kinyume na kumbukumbu za hapo nyuma, ambapo watu walikusanyika katika uwanja wa kitaifa wa Amahoro wakati huu sherehe zitafanyika katika maeneo ya vijijini.
Ni miaka 19 tangu mauaji hayo kufanyika na wanyarwanda wanajaribu kuyasahau mauaji mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo mwaka 19994 ambayo yaliwaacha zaidi ya watu milioni moja wakiwa wameuawa
Shughuli za mapatano miongoni mwa waathiri wa wa mauaji ya kimbari
Hata hivyo nchi hiyo imeweza kujikwamua na kugeuka kuwa mmoja ya mataifa yanayokuwa kwa kasi kubwa barani Afrika.
Huku Rwanda ikiwa bado inawakumbuka waliofariki katika mauaji hayo, baadhi ya washukiwa wakuu wa mauaji yenyewe wangali mbioni
Rwanda imetoa vibali vya kukamatwa kwa washukiwa 130 kote duniani ambao wanaendelea kukimbia. Mmoja wao ni Felicien Kabuga, anayetajwa kama mfadhili mkuu wa mauaji hayo.
Wengine ni pamoja na Protais Mpiranya, Augustin Bizimana, Fulgence Kayishema, Pheneas Munyarugarama, Aloys Ndimbati, Ladislas Ntaganzwa, harles Ryandikayo, and Charles Sikubwabo.
Washukiwa wengine kama Leon Mugesera na Jean Uwinkindi, wamekamatwa na kurejeshwa Rwanda.
Rwanda pia imetoa vibali 27 vya kuwakamata washukiwa wakuu kwa nchi za kigeni na kufikia sasa washukiwa kadhaa wameshakamatwa.

Taarifa zinazohusiana

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire