Kikosi cha MONUSCO nchini DRC
congovision.com
Umoja wa mataifa unaandaa kikosi imara cha uvamizi chenye askari 2000 kukabiliana na makundi ya wapiganaji wanaochochea machafuko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maofisa wa umoja huo, Tanzania na Afrika Kusini zinaongoza kampeni ya kutoa kikosi maalum cha kwanza kusaidia kikosi maalum cha Umoja wa mataifa kinacholinda amani nchini DRC.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa , limeidhinisha matumizi ya ndege zisizokuwa na marubani Mashariki mwa DRC, ambako kundi la waasi wa M23 waliteka jimbo muhimu la Goma mnamo mwezi Novemba mwishoni.
Kikosi hicho cha uvamizi na ndege zisizo na rubani zinaweza kuwa katika operesheni ndani ya miezi mitatu, afisa wa Umoja wa Mataifa alisema kwa masharti ya kutokujulikana.
Kazi kubwa ya ndege hizo itakuwa kufuatilia mpaka wa DRC na Rwanda, ambaYo wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaishutumu kwa kuwafadhili waasi wa kundi la M23 dhidi ya serikali, Madai ambayo Rwanda imeyakanusha.
Marais wa DR Congo, Rwanda, Burundi, Uganda, Angola, Jamhuri ya Kongo, Afrika Kusini na Tanzania zinataraji kuweka saini mkataba ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa, kuzindua upya juhudi za kisiasa na kuleta amani katika ukanda huo wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa siku ya Jumatatu.
Kikosi cha umoja wa mataifa kinacholinda amani nchini DRC, MONUSCO, ni chombo kikubwa cha umoja huo wa kimataifa kinacholinda amani ambacho kwa sasa kina askari wapatao 17,000 na chini ya mamlaka ya baraza lake la usalama chombo hicho kinaruhusiwa kuwa na askari hadi 19,800.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire