lundi 21 octobre 2013

Jacques Bigirimana akabidhiwa usukani wa kukiongoza chama kikuu cha Upinzani nchini Burundi cha FNL huku Agathon Rwasa akipinga uteuzi huo

Jacques Bigirimana kiongozi mpya wa chama cha FNL tawi linalo tambulika na serikali
Jacques Bigirimana kiongozi mpya wa chama cha FNL tawi linalo tambulika na serikali

Na Ali Bilali
Chama cha uasi zamani nchini Burundi cha FNL, kimefanya mageuzi kwenye uongozi wake na kumchaguwa katibu wake mkuu Jacques Bigirimana kuwa mwenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Jumapili Octoba 20 jijini Bujumbura. Uchaguzi huo umetupiliwa mbali na kinara wa zamani wa chama hicho Agathon Rwasa anaye amini na wengi kuwa ndiye kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa FNL.

Jacques Bigirimana amechaguliwa kwa asilimia zaidi ya sabini dhidi ya mtangulizi wake Emmanuel Miburo ambaye amepata chini ya asilimia ishirini ya kura.

Kulingana na sheria za taifa hilo Jacques Birimana ndiye kiongozi mkuu wa upinzani baada ya kuchaguliwa na wafuasi wa chama hicho.
Mwenyekiti huyo mpya ameviambia vyombo vya habari muda mfupi baada ya uteuzi wake kwamba chama chake hakitakuwa na upinzani wenye msimamo mkali kwani haifaikuw ana msimamo mkali na kwamba wataendesha chama hicho kwa kuwajibika na kumsikiliza kila mtu na kujaribu kuuwanisha pande zote.
Hata hivyo kulikuwepo na jambo lisiloeleweka baina ya wafuasi hao kwani wengi walisikika wakiimba nyimbo za kumsifu Agathon Rwasa kiongozi wa Kihistoria wa chama hicho na ambaye wengi wanaamini kwamba bado anaushawishi mkubwa na kwamba ndiye kiongozi halali wa chama hicho.
Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kiongozi huyo, Jacques Bigirimana alionekana kubadilika na kuwa na ghadhabu na kuhoji kwanini wamemuuliza swali hilo, na huenda labda wametumwa na kiongozi huyo.

Akizungumza kuhusu uteuzi huo wa Jacque Bigirimana kwenye uongozi wa chama hicho Agathon Rwasa ambaye bado anaumaarufu mkubwa katika chama hicho licha ya kuonekana kutengwa, amesema huo ni upinzani vibaraka wa serikali na kwamba hakuna kuwajibika kokote mbali na kuendelea kuunga mkono jitihada za kuubana upinzani wa ukweli.

Hata hivyo Uwala wa Bujumbura naendelea kumyima nafasi Agathon Rwasa ya kufanya shughuli yoyote ile kwa niaba ya chama FNL ukidai kwamba hana uhali wa kutumia chama hicho

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire