mercredi 18 mars 2015

Macky sall amtolea wito Kabila kuwaachilia raia wake

rais wa Senegal, Macky Sall, amtolea wito rais Joseph Kabila kuingila kati ili wanaharakati wa shirika la Y'en a marre wanaozuiliwa DRC waachiliwe huru.
rais wa Senegal, Macky Sall, amtolea wito rais Joseph Kabila kuingila kati ili wanaharakati wa shirika la Y'en a marre wanaozuiliwa DRC waachiliwe huru.
REUTERS/Joe Penney

Na RFI
Rais wa Senegal Macky Sall amemtaka mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila kuingilia kati ili wanaharakati wa vuguvugu la Y'en a marre wa Senegal wanaozuiliwa jela mjini Kinshasa waachiwe huru.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dakar hapo jana, rais huyo amesema kuwa yeye mwenyewe amepanga kuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na rais Kabila akitumia nafasi yake kama rais wa jamhuri ya Senegal.

Macky Sall amesisistiza kuwa moja ya majukumu yake ni kuhakikisha kwamba wanachama wa vuguvugu hilo la " Y'en Marre " kutoka Senegal wanaachiwa huru wote na wanarejea nyumbani.
Wakati hayo yakijiri, viongozi na nchi kadhaa duniani wamepaza sauti zao kuelezea wasiwasi wao kuhusu kukamatwa kwa wanaharakati hao ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Ufaransa na hususan Ubelgiji ambayo wanadiplomasia wake wanatarajiwa kuwasili mjini Goma siku ya Alhamis ambapo raia wake wawili wameshikiliwa mjini humo.

Itakumbukwa kwamba siku ya Jumapili, takriban watu 30 wakiwemo wanaharakati wa Y'en a marre kutoka Senegal, na balai Citoyen kutoka Burkina faso na baadhi ya wanaharakati na waandishi, raia wa Congo wametiwa mbaroni mjini Kinshasa ambapo walikuwa wakiendesha kongamano kuhusu Demokrasia na Utawala bora barani Afrika.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire