jeudi 25 septembre 2014

LA CENCO S'OPPOSE A LA REVISION DE LA CONSTITUTION EN EDC

DRC: Cenco yapinga jaribio la marekebisho ya baadhi ya Ibara za Katiba

Baraza kuu la maaskofu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Cenco limejiondoa kwenye Kamati ya uadilifu na maridhiano nchini DRC.
Baraza kuu la maaskofu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Cenco limejiondoa kwenye Kamati ya uadilifu na maridhiano nchini DRC.
cenco.cd

Na RFI
Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inapinga marekebisho yoyote ya Ibara ya 220 ya Katiba ya nchi hiyo kulenga mabadiliko ya mihula miwili ya rais kama inavyoandikwa katika katiba ya Congo.

Katika waraka wa maaskofu wenye jina la "kulinda taifa" na uliosomwa mbele ya vyombo vya habari, Baraza kuu la maaskofu wa Congo wanaonya kuwa jaribio lolote la kubadilisha ibara hiyo ni kupiga hatua nyuma katika jitihada za kuimarisha demokrasia na kuhatarisha mustakbali wa nchi.

Baraza kuu la maaskofu nchini Congo (Cenco) yapinga jaribio la marekebisho ya baadhi ya Ibara ya Katiba
cenco.cd
Aidha, sambamba na kauli hiyo, maaskofu hao wameamua kujiondoa kwenye Kamati ya uadilifu na maridhiano inayofanya kazi bega kwa bega na Tume ya uchaguzi, kama ishara nyingine kwamba Kanisa Katoliki halitaki kuidhinisha mchakato wa uchaguzi ambao uko kinyume na sheria za nchi.

Kwa upande wake, serikali ya DRC imejibu kwamba maaskafu hao wamefanya maamuzi na kutoa kauli kama na hizo kwa kujibu hoja ambazo hazijawekwa mezani.

Lambert Mende, waziri wa habari akiwa pia msemaji wa serikali ya Congo.
©RFI/Delphine Michaud
Waziri wa mawasiliano wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo akiwa pia msemaji wa serikali, Lambert Mende, amesema kutoelewa kwanini Baraza hilo la maaskofu limeharakia kuchukua uamzi wakati Ibara hiyo haijajadiliwa .
“Naendelea kusisitiza kuwa hapa tulipofikia, hakuna hatua yoyote ya kisheria au ya kitaasisi iliyoamua marekebisho ya Ibara 220. sielewi maaskofu wanahisi furaha kiasi gani kujadili hoja ambazo hajiwekwa mezani”, amesema Lambert Mende.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire