DRC: Raia waandamana mjini Goma
Joseph KabilaRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila.
(Photo: AFP)
Jeshi la jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Wakaazi wa
Mashariki mwa taifa hilo wanaomboleza kifo cha Meja Jenerali Lucien
Bauma Ambamba.
Afisa huyo wa ngazi ya juu katika jeshi ambaye alikuwa katika
mustari wa mbele kupambana na waasi wa mashariki mwa nchi hiyo hususan
waliokuwa waasi wa M23 na ADF/NALU.Kifo chake kilitokea nchini Afrika Kusini mwishoni mwa juma lililopita, baada ya kusafirishwa kwa dharura kutoka nchini Uganda alipokuwa katika mkutano wa viongozi wa kijeshi alhamsi iliopita jijini Kampala na kukumbwa na maradhi ya kiharusi.
Kifo cha meja jenerali Lucien Bahuma kimesababisha kuzuka kwa maandamano ya raia na wake wa askari mjini Goma wakati huu mashirika ya kiraia yakitowa wito wa kufanyika uchunguzi.
Hata hivo serikali ya jimbo la Kivu Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetoa wito kwa raia wa eneo hilo kuwa watulivu baada ya maandamano na hisia tofauti zilizofwatia kifo cha Jenerali Lucien Bauma Ambamba, kamanda mkuu wa mkoa wa kijeshi wa Kivu Kaskazini mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Gavana wa Mkoa wa Kivu ya Kaskazini Julien Paluku, amewatolea wito wa amani wananchi wa eneo hilo ambao wameandamana
Kifo hicho kinatokea miezi nane baada ya kifo cha Kanali Mamadou Ndala Mustapha kiongozi mwingine wa kijeshi wa eneo hilo alieuawa katika mazingira ya kutatanisha, na hivo kuwafanya watu kutoamini kwamba jenerali Bahuma amefariki kutokana na maradhi.
Kanal
Mamadou Ndala Moustafa ,akiwa na kikosi cha wanajeshi wake katika
kijiji cha Kokola, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia uya Congo, , Desemba
31 mwa 2013.
AFP / ALAIN WANDIMOYI |
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire