DRC: wabunge kutoka upinzani watishia kususia vikao vya Bunge
Etienne
Tshisekedi (kushoto) pamoja na Vital Kamerhé (kulia), viongozi wawili
wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
AFP/ Montage RFI
Wabunge kutoka vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na waanowakilisha vyama kadhaa wametangaza nia yao
ya kususia mijadala ya Bunge inayoendelea kuhusu marekebisho ya katiba.
Chama cha pili cha upinzani kwa ukubwa nchini humo cha UNC cha
bwana Vital Kamerhe na chama kikuu cha upinzani cha UDPS cha Etienne
Tshisekedi bado baadhi ya wabunge wao wanaendelea kuwepo bungeni, huku
wawakilishi wao katika tume huru ya uchaguzi wakiwa tayari wamejiondoa
katika tume hiyo.
Madhumuni ya hatua hiyo kwa muda ni kuishinikiza serikali ya kinshasa kuachana na mpango wake wa kurekebisha katiba na kutaka mazungumzo ya kina na serikali hiyo, kama alivyobainisha Vital Kamerhe mwenyekiti wa chama cha upinzani cha UNC nchini DRC.
Katika hatua nyingine mashirika ya kiraia yameunga mkono tamko la maaskofu nchini drc kuhusiana na mabadiliko ya katiba yanayotarajiwa kufanyika.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire