31 Machi, 2013 - Saa 14:49 GMT
Katika sala ya Pasaka mjini Nairobi rais mteule, Uhuru Kenyatta, aliwataka Wakenya waombe amani:
"nachukua fursa hii kuwashukuru Wakenya wote kwa kuweka amani tangu kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi; na naendelea kuwaomba Wakenya kuomba amani, kwa sababu amani ndiyo itatupa uwezo wa kufanikiwa; na hiyo amani ndiyo itatuwezesha sote kufikia ndoto zetu, malengo yetu na matumaini ya Wakenya wote, popote walipo."
Huku nyuma polisi walipambana na waandamanaji wachache mjini Kisumu kwenye wafuasi wengi wa Raila Odinga ambaye Jumamosi alikataliwa malalamiko yake kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais, ambapo Uhuru Kenyatta alishinda.
Ghasia zilizotokea Jumapili ni ndogo tu baada ya ghasia za Jumamosi usiku, ambapo watu wawili walikufa mjini humo.
Inaarifiwa ghasia za Jumapili ni katika vitongoje tu vya Kisumu na polisi wanasema hali imedhibitiwa.
Bwana Odinga alisema Jumamosi usiku kwamba anaheshimu uamuzi wa mahakama, lakini ataangalia njia nyengine za salama za kutafuta suluhu.
Aliwaomba wafuasi wake waepukane na umwagaji damu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire