8 Aprili, 2013 - Saa 06:04 GMT
Afrika Kusini imetangaza kuwa
itatuma wanajeshi Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kujumuika katika kikosi
maalumu cha Umoja wa Mataifa cha kuingilia kati nchini humo ili
kuwanyan'ganya silaha wapiganaji.
Taarifa hiyo imetolewa majuma machache tu baada
ya wanajeshi 13 wa Afrika Kusini kuuwawa Jamhuri ya Afrika ya Kati
katika hali ya kutatanisha.Upande wa upinzani umelaani mpango huo, wanasema kuwa haukufikishwa mbele ya bunge.
Waziri kivuli wa Ulinzi wa chama cha Democratic Alliance, David Maynier, alisema kuna hatari ya wanajeshi zaidi kupoteza maisha yao.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa idhini mwisho wa mwezi uliopita kutuma kikosi kitachoweza kupigana na kuingilia kati katika Congo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire