vendredi 24 octobre 2014

BURKINA: LE CRIMINEL QUI A ASSASSINE THOMAS SANKARA NE VEUT PAS QUITTER LE POUVOIR APRES 27ANS

Burkina Faso: Upinzani waanzisha kampeni dhidi ya kura ya maoni

Kwa sasa Katiba ya Burkina faso haimruhusu rais Blaise Compaoré kugombea katika uchaguzi wa rais.
Kwa sasa Katiba ya Burkina faso haimruhusu rais Blaise Compaoré kugombea katika uchaguzi wa rais.
REUTERS/Noor Khamis

Un assassin criminel de Sankara cherche le pouvoir à vie auprès des dirigeants français, les commanditaires des crimes en Afrique
Na RFI
Upinzani nchini Burkina Faso umeamua kuanzisha kampeni ya kuhamasisha raia kupinga zoezi la kupiga kura ya maoni, ambayo serikali inapanga kuitisha ili kuifanyia marekebisha Ibara ya 37 ya Katiba.

Hivi karibuni serikali imepitisha muswada wa sheria kuhusu kuongeza au kupunguza idadi ya mihula ya rais madarakani. Lakini upinzani unaona kwamba ni mbinu za serikali za kutaka kumuungezea muhula rais Blaise Compaoré, ili asalie madarakani.
Rais Blaise Compaoré ametimiza miaka 27 akiwa madarakani. Upinzani umesema kampeni hiyo ya kuhamasisha raia kupinga zoezi la kupiga kura itaanza kwa maandamao ya siku nzima Jumanne Oktoba 28.
Upinzani umebaini kwamba kampeni hiyo haitositishwa hadi pale serikali itaachana na mpango huo wa kutaka kuzifanyia marekebisho baadhi ya Ibara za katiba.
Upinzani umesema unapinga mpango huo wa serikali ambao umeuita “mapinduzi ya katiba”. Kwa mujibu wa Zéphirin Diabré , kiongozi wa upinzani, maandamano hayo yatafanyika nchi nzima.
Zéphirin Diabré, amewaomba wabunge kushirikiana na upinzani katika kampeni hiyo dhidi ya marekebisho ya Katiba.
“ Upinzani unawatolea wito wabunge wazalendo wanaohitaji amani na uhuru kuonesha msimamo wao na kupuuzia utumwa”, amesema Zéphirin Diabré.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire