mardi 4 février 2014

Uganda yakanusha kufadhili kundi la waasi wa M23

Yoweri Kaguta Museveni, rais wa Uganda
Yoweri Kaguta Museveni, rais wa Uganda
RFI

Na RFI
Serikali ya Uganda imekanusha madai yanaondelea kutolewa na shirika la Umoja wa Mataifa UN kwamba inaendelea kusaidia kundi la M23 huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata kusema huo ni upuzi mtupu na itaendelea na juhudi zake za kuona kuwa usalama unadumishwa kwenye kanda nzima ya maziwa makuu.

Hayo yakijiri, ujumbe wa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO umekamilisha ziara yake ya siku 4 nchini Uganda kutathmini makambi ya waasi wa zamani M23 .

Ziara hii inafuatia ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa ya hivi karibuni ambayo inadai kuwepo kwa "habari za kuaminika " kuwa waasi hao wanajipanga upya kuivaamia tena DRC, jambo ambalo halikuthibitishwa na Ujumbe Huo.

Naibu mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Abdullah Wafi, ambae pia alikua akiongoza ujumbe huo wanajiandaa kushirikiana na wahusika wote katika mzozo wa Congo ili ufumbuzi upatikane.
“Kiukweli sijaona watu wakijipanga, nadhani kwamba kilicho cha msingi ni kuchukuwa fursa hii kutoka nchi ya Uganda ili tuunde pamoja tume kwa kukabiliana na kesi zote hata za wale walioko kwenye orodha ya vikwazo ili tupate suluhu kulingana na sheria za kimataifa na wadau wote walioshiriki.

Kundi la waasi la M23 lilitumuliwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka uliyopita, baada ya kushindwa mapigano kati yake na majeshi ya serikali, na kutangaza tarehe 11 mwezi wa julai mwaka 2013 wanasitisha uasi dhidi ya serikali ya Kinshasa.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire