mardi 5 novembre 2013

Hatimaye Kundi la uasi la M23 la tangaza kumaliza uasi, saa chache baada ya serikali kutangaza ushindi dhidi yake

DRC-M23 - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumanne 05 novemba 2013 - Taarifa za ivi karibuni : Jumanne 05 novemba 2013

Baadhi ya wapiganaji wa kundi la waasi la M23 lililotangaza kumaliza uasi Mashariki mwa DRC
Baadhi ya wapiganaji wa kundi la waasi la M23 lililotangaza kumaliza uasi Mashariki mwa DRC
reuters.com

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Kundi la uasi la M23 limetangaza kuweka silaha chini na kutamatisha uasi wake kuanzia leo Jumanne, saa chache baada ya serikali ya Kinshasa kutangaza ushindi dhidi yao.

Taarifa ya kundi hilo imeeleza kuwa wameamua kuanzia leo kutamatisha uasi na badala yake kundi limeamua kutekeleza malengo yake kwa njia za kisiasa.

Hatua hii inatamatisha uasi uliodumu kwa miezi 18 ambao umelikumba eneo la ukanda wenye utajiri wa madini eneo ambalo linazozewa barani Afrika kwa takribani karne mbili zilizopita.
Mapema jeshi la serikali lilitangaza ushindi dhidi ya kundi hilo baada ya kudhibiti milima miwili ya mwisho ya Runyonyi na Chanzu ambayo zilikuwa ngome zao za mwisho kufuatia shinikizo la wanajeshi wa FARDC waliofika katika maeneo hayo ya milima yaliyopo umbali wa kilomita 80 Kaskazini mwa mji wa Goma.
Msemaji wa serikali na waziri wa mawasiliano wa DRC Lambert Mende amesema kuwa hatimaye waasi hao wameamua kuweka silaha chini na kukimbia kutoka katika ngome zao za mwisho.
Aidha Mende amesema kuwa huo ni ushindi kwa DRC, na kuongeza kwamba waasi wengi wamekimbilia nchi jirani ya Rwanda
Jana Jumatatu kikosi maalumu cha jeshi la Umoja wa Mataifa UN Mashariki mwa DR Congo liliungana moja kwa moja na jeshi la Serikali dhidi ya waasi wa M23 kwa kutekeleza jukumu lao la kulinda raia wakati wa mashambulizi.
tags: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - Kundi la Waasi la M23

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire