jeudi 23 avril 2015

CONFIRME, LE RWANDA ATTAQUE DE NOUVEAU LA RDC, VIA BUNAGANA ET VIRUNGA

DRC: wanajeshi wa Rwanda waingia Kivu-Kaskazini

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakipiga doria, hapa ni katika hifadhi ya taifa ya wanyama ya Virunga, Desemba mwaka 2013.
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakipiga doria, hapa ni katika hifadhi ya taifa ya wanyama ya Virunga, Desemba mwaka 2013.
REUTERS/Kenny Katombe

Na RFI
Hali tete yaripotiwa mkoani Kivu-Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya wanajeshi wa Rwanda kuvuka mpaka na kuingia katika ardhi ya nchi hiyo. Sababu mpaka sasa bado hazijajulikana.

Viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasaia ya Congo wamethibitisha Jumatano Aprili 22 kuingia kwa wanajeshi wa Rwanda katika ardhi ya Congo, kilomita 120 kaskazini mashariki mwa mji wa Goma, katika hifadhi ya taifa ya wanyama ya Virunga, hifadhi ambayo inapanuka hadi kwenye mpaka wa Congo na Rwanda.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Kivu-Kaskazini, Julien Paluku, Jumatano Aprili 22, wanajeshi wa Congo wakiandamana na walinzi wa hifadhi ya taifa ya wanyama ya Virunga wamethibitisha kuwepo kwa wanajeshi wa Rwanda katika kijiji cha Musangoti, karibu mita 1,000 katika ardhi ya Congo. Eneo ambalo ni sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Virunga, kwenye umbali wa kilomita 100 kaskazini mwa Goma
Wakati huohuo wanajeshi wa Rwanda waliwarushia risasi wanajeshi wa Congo, ameeleza mkuu wa mkoa wa Kivu-Kaskazini. Hata hivyo Julien Paluku amechukua utaratibu wa pamoja kwa minajili ya uchunguzi.
Mkuu wa Mkoa wa Kivu-Kaskazini atakua na uwezo wa kuchunguza tangu leo Alhamisi iwapo kuna wanajeshi wa Rwanda katika eneo hilo au la.
Kama vyanzo rasmi vimethibitisha kuwepo kwa wanajeshi wa Rwanda katika kijiji hicho cha Rutshuru, wakaazi wa kijiji hicho wamebaini kuwepo kwa watu wengine wenye silaha wakivalia sare ya jeshi kusini, kuelekea Goma.
Karibu na kijiji cha Ehu, kilomita thelathini kutoka Goma, wanajeshi kadhaa wa Rwanda walivuka mpaka usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili na kuelekea katika hifadhi ya taifa ya wanyama ya Virunga. Taarifa hii iliyotolea na mashahidi haijaweza kuthibitishwa na viongozi wa Congo. Si mara ya kwanza wanajeshi wa Rwanda kuingia katika ardhi ya Congo. Mwezi Juni, majeshi kutoka nchi hizi mbili zilirushiana risasi katika eneo la mpaka lililogawiwa vibaya.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire