vendredi 10 janvier 2014

Rwanda yakanusha uvumi kuhusu kifo cha Rais Paul Kagame

Paul Kagme, rais wa Rwanda
Paul Kagme, rais wa Rwanda
RFI

Na RFI
Ikulu ya rais wa Rwanda imekanusha leo ijumaa uvumi kuhusu kifo cha rais Paul Kagame, ambao umepelekea raia wa mji wa Goma kuandamana mabarabarani wakisheherekea kwa furaha taarifa hio. Rwanda iliingia kijeshi mara kadhaa kwenye aridhi ya Congo, hasa ikiwaunga mkono waasi dhidi ya utawala wa Kinshasa wakati wa vita viliyoibuka nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiitwa Zaïre wakati huo, katika miaka ya 1996-1997 na katika miaka ya 1998 hadi 2003.

Rwanda imeelezea mshangao wake kuona uvumi huo ukizagaa, huku raia wa mashariki ya Congo wakiandamana wakionyesha furaha kuhusiana na na taarifa isiyokua ya kweli.
Afisa m'moja anaefanya kazi kwenye Ikulu ya rais wa Rwanda, amefahamisha AFP kwamba taarifa ya kifo cha rais Paul Kagame ilikua uvumi mtupu.
“ Rais wakati huu tunaongea, anakutana kwa mazungumzo na wanafunzi wa chuo kikuu kutoka Marekani. Muko huru kuja kuhudhuria kikao hicho, na muweze kukutana nae, ameendelea kusema afisa huyo.
Paul Kagame, mwenye umri wa miaka 56, ni rais wa Rwanda tangu mwaka wa 1994, baada tu ya waasi wa RPF kushinda jeshi la Rwanda lilokua likimuunga mkono rais Juvenal Habyarimana. Chanzo cha kushindwa kwa jeshi la Rwanda ni mauaji ya kimbari, ambayo lilihusishwa jeshi hilo.
Watu laki nane, wengi wao kutoka jamii ya watutsi waliuawa.
Wafuasi wa rais Paul Kagame wanamsifu kwamba ni mtu mwenye mtazamo katika masula ya uchumi, na lengo lake ni kuliendeleza taifa la Rwanda, huku wapinzani wake wakimtuhumu kujihusisha na tabia mbovu ya kufuta vyama vya upinzani.
Paul Kagame amevaa lawama, kwa mujibu wa Jumuiya ya Kimataifa, kutokana na kuunga mkono makundi ya wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya kua Kigali imeendelea kukanusha madai hayo.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire