M23-DRC-UGANDA -
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumanne 10 septemba 2013 -
Taarifa za ivi karibuni : Jumanne 10 septemba 2013
Renee Abandi, mkuu wa ujumbe wa M23 kwenye mazungumzo ya Kampala
Reuters
Mazungumzo ya amani kati ya waasi wa M23 na upande wa
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC yanatarajiwa kuanza
hii leo mjini Kampala, Uganda kusaka suluhu ya mzozo wa mashariki mwa
nchi hiyo.
Mazungumzo haya ambayo yanakuwa ni ya pili kufanyika baada ya
yale ya awali kuvunjia bila kupatikana suluhu, yanakuja kufuatia
maazimio ya viongozi wa nchi 11 za maziwa makuu kutaka pande hizo mbili
kurejea kwenye meza ya mazungumzo.
Tayari ujumbe wa M23 unaoongozwa na Renee Abandi umeshawasili mjini Kampala toka mwishoni mwa juma ukisisitiza utayari wake wa kumaliza machafuko mashariki mwa nchi hiyo.
Hapo jana mkuu wa kundi la M23, Betrand Bisimwa alitoa mashrti ya kundi lao kusalimisha silaha akidai kuwa watafanya hivyo iwapo kundi la FDLR litafurushwa nchini humo pamoja na wakimbizi wa kongo kurejea nyumbani.
Masharti haya ambayo yanaonekana ni mapya na yanayoweza kutekelezeka yanakuja wakati huu ambapo Serikali ya Kinshasa imeonesha wasiwasi wake kuhusu kusitisha vita dhidi ya kundi ikidai kuwa kutatoa mwanya wa kundi hilo kujipanga upya.
Mpaka sasa haijajulikana ni lini hasa mazungumzo haya yataanza kwakua ujumbe wa Serikali ya Kinshasa bado haujawasili mjini Kampala wala haijajulikana utaongozwa na nani.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire