Kutoka kushoto ni rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda Yoweri Museveni na rais wa DRC Joseph Kabila wakati walipokutana hivi karibuni
Reuters
Na Emmanuel Richard Makundi
Viongozi wa kundi la waasi wa M23 na wale wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wanatarajiwa kuwa na mkutano wao hii leo mjini Kampala Uganda, mazungumzo yanayolenga kumaliza tofauti zao.
Kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Jean-Marie Runiga na Betrand Bisimwa wanahudhuria mkutano huo kama wawakilishi wa kundi lao kujaribu kuishawishi Serikali ya DRC kukubaliana na matakwa yao.
Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaongozwa na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Raymond Tshibanda ambaye amewaambia waandishi wa habari kuwa anaimani waasi wa M23 watakubaliana na mapendekezo ya Serikali yake.
Rais Josephu Kabila hatohudhuria mkutano huo wa kampala kwakuwa atakuwa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ambako anahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC abao nao watajadili hali ya mambo nchini DRC.
Mazungumzo haya ya awali yanalenga kutazama namna ya kufanya mazungumzo yenyewe na kuteua watu ambao watakuwa wakishuhudia mazungumzo hayo yakiendelea na kuwa kama waangalizi wa yale yatakayokuwa yanajiri kwenye mkutano wao.
Serikali ya Uganda imeapa kuhakikisha inafanikisha mazungumzo ya safari hii na kwamba kundi la waasi wa M23 na wale viongozi wa Serikali ya DRC wataafikiana kmaliza tofauti zao ili kuleta manai mashariki mwa nchi hiyo.
Majuma kadhaa yaliyopita kundi la M23 lilikuwa limeushikilia mji wa Goma kabla ya mwishoni mwa juma lililopita kutangaza kuondoka baada ya mazungumzo ya kampala na viongozi wa wakuu wa nchi za Ukanda wa maziwa makuu ICGLR ambao waliwataka waasi hao kuondoka kabla ya kuanza kwa mazungumzo.
Jumuiya ya kimataifa tayari imewawekea vikwazo baadhi ya viongozi wa kundi la M23 akiwemo kiongozi wake Sultan Makenga na Bosco Ntaganda ambaye anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire