Wapiganaji wa Kundi la M23 wakiondoka kwenye mji wa Goma nchini DRC
Reuters
Waasi wa kundi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao majuma kadhaa yaliyopita yalikuwa yanaushikilia mji wa Goma na kisha juma lililopita kuondoka kwenye mji huo, wameapa kurejea kwenye mji huo iwapo Serikali ya DRC haitafanya mazungumzo nao.
Kuondoka kwa majeshi ya waasi kwenye mji wa Goma kumekuja baada ya kumalizika kwa mkutano wa wakuu wa nchi za ukanda wa maziwa makuu ICGLR uliofanyika mjini Kampala Uganda ambapo viongozi wa nchi 11 wanachama waliazimia kudni hilo kuondoka mjini Goma kupisha mazungumzo.
Licha ya kundi hilo kuondoka kabisa kwenye mji wa Goma bado Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imesisitiza kutokufanya mazungumzo na waasi wa kundi hilo kwakuwa madai yao hayatekelezeki.
Moja ya masharti ya kundi hilo ni kutaka kupewa umiliki wa mji wa Goma na kutengeneza Serikali yao pamoja na kuitaka Serikali kutekeleza maazimio ya mwaka 2009 iliyotia saini kati yake na makundi ya waasi.
Katika hatua nyingine licha ya waasi ho kuondoka kwenye mji wa Goma bado hali imeendelea kuwa tete kwenye mji huo kufuatia kuripotiwa kwa matukio ya watu wenye silaha kushambulia kambi za wananchi ambao hawana makazi.
Mbali na mashambulizi kwenye kambi za wakimbizi, pia kumeripotiwa mapigano makali kwenye mpaka wa Rwanda na DRC ambapo waasi wenye asili ya Kihutu wameelezwa kupigana na majeshi ya Rwanda.
Kwa mujibu wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR limesema kuwa kumeripotiwa matukio ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kwenye kambi za Mugunga kambi ambayo iko umbali wa kilimeta 10 mashariki mwa mji wa Goma.
Zaidi ya watu elfu 35 hawana makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kuharibiwa kutokana na mapigano.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire