jeudi 26 février 2015

KAGAME à Paris cette semaine à l'absence de Hollande et Valls

Que cherche Kagame à Paris à l'absence du président  Hollande et Valls? 

On sait que cet homme vit au dépend des USA et UK. Il a des pseudo discours panafricains mais est un pire marionnette des Anglosaxons.

Kagame atazamiwa kuwasili Ufaransa

Ziara ya Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, Alhamisi Februari 26 mwaka 2015, lakini hakuna mkutano ambao umepangwa kufanyika kati yake na viongozi wa Ufaransa.
Ziara ya Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, Alhamisi Februari 26 mwaka 2015, lakini hakuna mkutano ambao umepangwa kufanyika kati yake na viongozi wa Ufaransa.
REUTERS/Ruben Sprich

Na RFI
Rais wa Rwanda Paul Kagame anatazamiwa kuwasili Alhamisi wiki hii mjini Paris, nchini Ufaransa, kwa mwaliko wa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya sayansi na utamaduni Unesco, katika wiki mahsusi iliyoandaliwa kwa minajili ya teknolojia mpya na mchango kwa maendeleo na elimu ya wanawake hasa.

Ni kwa mara ya kwanza rais wa Rwanda Paul Kagame anaweka mguu wake katika aridhi ya Ufaransa tangu aituhumu nchi hio kuwa ilishiriki katika mauaji ya kimbari yaliotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Karibu mwaka mmoja baadaye, hakuna mikutano baina ya rais wa Rwanda na viongozi waandamizi wa Ufaransa iliyofanyika.
Rais wa Rwanda atawasili Ufaransa, lakini hakupanga kukutana na viongozi wa nchi hii. Hata hivyo rais wa Ufaransa François Hollande, na waziri wa mambo ya nje Laurent Fabius hawako nchini ili kuweza kukutana na Paul Kagame, duru kutoka viongozi wa Ufaransa zimebainisha.
Paul Kagame anakuja kwa mwaliko wa Unesco wala sio ziara atakayoifanya nchini Ufaransa, jamii ya raia wa Rwanda waishio Ufaransa imesema.
Tangu mkutano kati ya Paul Kagame na Laurent Fabius, katika mji mkuu wa Gabon, Libreville, chini ya mwamvuli wa Ali Bongo ilikuwa kwenye mkutano wa 3 wa New York Forum Africa mwezi Mei, hakuna jitihada za kidiplomasia zilizofanywa kati ya nchi hizo mbili. Katika kikao hicho , Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa alimuomba rais wa Rwanda aonyeshe ushahidi tosha unaothibitisha kuwa ufaransa ilishiriki moja kwa moja katika mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.
Paul Kagame alijibu kwamba atamuandikia barua François Hollande. Lakini mpaka sasa barua hio bado inasubiriwa. Ufaransa ndio iko katika kosa, ni kwa nchi hio sasa kufanya juhudi, chanzo cha rasmi cha Rwanda kimeeleza. Mzozo huo unajitokeza baada ya miaka sita ya kukwama kwa uhusiano kati ya nchi hizi mbili.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire