Baadhi
ya wapiganaji waasi wa kundi la M23 ambao wamekuwa wakisababisha
machafuko mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo
RFI
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya jamuhuri ya
demokrasia ya Congo,na kundi la waasi wa M23 yameahirishwa kwa mara
nyingine jumatatu pamoja na kwamba Umoja wa Mataifa UN ulishinikiza
hatua hiyo ili kufanikisha amani ya mashariki mwa nchini hiyo.
Pande zote mbili zilitangaza kusitisha mazungumzo hayo ya amani
yaliyokuwa yakiendelea mjini Kampala nchini Uganda muda mfupi baada ya
mjumbe wa Umoja wa mataifa kuonya juu ya hatari itakayotokea ikiwa
mpango wa makubaliano hautafikiwa mara moja kukomesha mapigano katika
eneo la mashariki mwa nchi hiyo.Msemaji wa serikali ya Congo DR Lambert Mende alibainisha kuwa mazungumzo yaliahirishwa baada ya kutokuwa na makubaliano juu ya kiwango cha msamaha kwa waasi wa m23 na ushirikishwaji katika jeshi la Congo FARDC.
Mjumbe wa waasi wa M23 Roger Lumbala amesema kuna kikwazo huku akisisitiza kuwa waasi wapo radhi kurejelea mazungumzo wakati wowote.
Serikali mapema ilitoa onyo kwamba mazungumzo ambayo yaliendelea mwezi septemba kwa shinikizo la wakuu wa Umoja wa Mataifa ya Afrika yalielekea kushindwa.
Wajumbe maalum wa Umoja wa Mataifa alitoa UN wamearifu mapema jumatatu kuhusu kukosekana kwa mpango wa msingi wenye lengo la kukomesha mapigano yanayosababishwa na kundi hili la waasi wa m23 ambao wamesababisha hali ya sintofahamu katika nchi hiyo yenye utajiri wa madini.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire