Jumamosi 24 agosti 2013
Mapigano mapya yazuka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo DRC huku shinikizo la kuchukunguzwa kama silaha za kemikali
zimetumika nchini Syria likizidi
Wanajeshi
wa Jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC wakiwa
kwenye doria katika Mji wa Goma kukabiliana na Kundi la Waasi la M23
Reuters
Kikosi cha Umoja wa Mataifa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo MONUSCO kimeamua kuingilia kati mapigano mapya
yaliyozuka Mashariki mwa DRC kwa kutoa usaidizi kwa Jeshi la FARDC
linalopambana na Kundi la Waasi la M23, Hali ya wasiwasi imeendelea
kutamalaki nchini Misri kipindi hiki Kiongozi wa zamani wa Taifa hilo
Hosni Mubarak akiachiwa kwa masharti huku Viongozi wa Chama Cha Muslim
Brotherhood wakiendelea kushikiliwa na Mataifa ya Magharibi wamezidisha
shinikizo kwa Serikali ya Syria kukubalia kufanyika kwa uchunguzi
kubaini iwapo shambulizi lililotekelezwa kwenye viunga vya Damascus kama
lilitumia silaha za kemikali!!
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire