Jumamosi 20 julai 2013
Mapigano makali yazuka nchini DRC kati ya Wanajeshi wa FARDC na
Wapiganaji wa Kundi la M23 kipindi hiki Marekani ikichungulia kuingia
kwenye mgawanyiko wa kibaguzi wa rangi
Wanajeshi
wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC wakiwa kwenye
mapambano na Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 huko Kivu Kaskazini
REUTERS/Kenny Katombe
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC limefanikiwa
kuwadhibiti Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 kwenye mapambano makali
yaliyoshuhudiwa Jimboni Kivu Kaskazini na kuchangia dhidi ya wapiganaji
wake mia moja ishirini na wanajeshi kumi wakipoteza maisha, Wananchi wa
Misri wameendelea kugawanyika kwa misingi ya kisiasa kutokana na wafuasi
wa Mohamed Morsi kuendelea kushinikiza Kiongozi wao arudishwe
madarakani na kukataa kutambua mapinduzi yaliyofanyika, Rais wa Kwanza
Mzalendo nchini Afrika Kusini na Mpambanaji dhidi ya Ubaguzi wa Rangi
Nelson Mandela maarufu kwa jina la Mzee Madiba ametimiza miaka 95
alhamisi hii huku dunia ikienzi harakati zake na Taifa la Marekani
huenda likatumbukia kwenye mgawanyiko wa rangi kutokana na wamarekani
weusi kuoneshwa kukerwa kwa namna ambavyo hukumu zinatolewa na kuonesha
kuna chembechembe za ubaguzi!!
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire