lundi 5 août 2013

RAIS KIKWETE AWAPA WANYARWANDA SIKU 14 ZA KUONDOKA TANZANIA.....MAMIA WAANZA KUREJEA RWANDA



Mamia ya wahamiaji haramu kutoka nchini Rwanda wakiwa na ng’ombe zaidi 900 wameanza kuondoka nchini kurejea kwao kutokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete kuwataka waondoke Tanzania kabla ya siku 14.  
                           
Traduction: Hundreds of illigal immigrants from Rwanda with  more than 900 Cows have started to leave Tanzanie and return home(Rwanda) as ordered by President Jakaya Kikwete that they  leave within 14 days.

Aidha, imeelezwa kuwa kumekuwapo ongezeko la askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mkoani Kagera hasa wilayani Ngara hali inayozua hofu kwa baadhi ya wananchi, huku ikiongeza msukumo kwa wahamiaji haramu kuondoka.

Traduction: There is a increase in numbers of tanzanian troops (TPDF) in the province of Kagera mainly in the district of Ngara. This situation has created fear among some Citizens while the pressure of pushing rwandese back to their country is increasing.Akiwa katika ziara mkoani Kagera, Rais Kikwete alitoa agizo la kuwataka wote waliokuwa wakiishi nchini kinyume cha sheria waondoke mapema jambo lililotakiwa kuanza kutekelezwa Julai 29 na kukamilika Agosti 10 mwaka huu.

While touring the province of Kagera, president Kikwete ordered all illigal individuals(immigrants)  to leave  before the implimentation of this order by July 29 till August 10 this year.Alisema kuwa wahamiaji haramu na wale wanaoendesha ama kuhusika na ujambazi, uhamiaji haramu na uingizaji haramu wa mifugo waamue kuchukua hatua mwafaka za kuondoka mapema kabla vyombo vya ulinzi na usalama kuanza operesheni maalumu ya kuwasaka.

He said that all iligal immigrants and those involved in criminalactivities , in cattles trafficking should decide to  take a wise decision to repatriate on time before our security and defence forcesstart the operation of searching for them.

Tayari idadi kubwa ya wafugaji wenye makundi ya ng’ombe imeanza kuondoka kuelekea eneo la mpakani la Rusumo kutoka ardhi ya Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa agizo hilo la Rais Kikwete.
Right now, a large number of farmers with a huge number of cows have started to move towards the border area of Rusumo in Tanzania as an implimetation of  president kikwete's order.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Costantine Kanyasu alisema kwamba idadi kubwa ya wafugaji waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria, imeitikia wito wa agizo la Rais na kuanza kuondoka kwa hiyari yao.
Hata hivyo, alisema kuwa pamoja na idadi kubwa ya wahamiaji kuanza kuondoka, bado wapo ambao hawajaondoka kutokana na kudai kuwa na vibali walivyovipata kutoka Ofisi ya Uhamiaji na kubainisha kwamba vibali hivyo vitakaguliwa kwa umakini wakati wa operesheni maalumu ili kujua uhalali wake.
Traduction: While talking to locals by phone on Sunday, the Ngara dictrict commissioner  Constantine kanyasu said that a large number of illigal farmers (with cows) have positively responded to the president's call as they have started to leave on their own will.
“Jambo hili la wahamiaji haramu lilikuwa kero kubwa, siyo tu kwa Wilaya ya Ngara, bali mkoa mzima wa Kagera, lakini tunashukuru sasa wameanza kuondoka, wamebaki hao wenye vibali. Ni lazima vibali hivyo tutavikagua maana vipo vilivyotolewa kinamna,” alieleza Kanyasu.
The problem of illegal immigrants have been a big issue to not only the district of Ngara but the entire province of kagera, we thank God that they have started to leave, only those with permits are staying. It is a must that we check( verify) those permits as some were issued fraudelently, said Kanyasu.
Alionya kwamba jukumu la kuwaondoa kwa nguvu wahamiaji haramu pamoja na wafugaji linasubiri muda wa mwisho ili kuanza kutekelezwa kama Rais Kikwete alivyoagiza.
She warned that the forced repatriation process for illegal immigrants and farmers is waiting to the deadline before its implimentation as ordered by president Kikwete.
Hofu ya Wanajeshi kuongezeka: Concern of seeing an increase in Army (troops) presence.
Akizungumzia suala la wanajeshi kudaiwa kuongezeka wilayani Ngara, Kanyasu alisema kwamba katika wilaya yake kuna kikosi cha dharura kinachokaa katika moja ya kambi za JWTZ kikikuwa na idadi kubwa ya askari lakini wananchi hawakuwa na taarifa nacho ila kutokana na sababu za kiusalama.
While talking to the issue of an increase in soldiers presence in the district if Ngara, Kanyasu said that in her district there has been a unit of rapid intervention in one of the Tanzanian People's Defence Forces (TPDF) with many soldiers but this was not disclosed to the public for security reasons.“Unajua kuna kelele za hapa na pale na haya majibizano yanayotokea baina ya Rwanda na Tanzania. Haya ni kama yamewastua watu na kudhani kuwa askari wetu wa Kikosi cha Dharura waliopo hapa Ngara wameletwa maalumu kutokana na tahadhari,” alisema na kufafanua kuwa askari hao wapo siku zote kwa ajili ya kulinda mipaka ya Tanzania. " You know there are rumours of here and there regarding the exchange between Rwanda and tanzania. It seems likes this has surprised people who think that our troops (TPDF) of intervention unit from is brought in from Ngara as a precaution," and added that those troops are always there to protect the tanzanian borders.Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kutulia na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
Despite that, the district commissioner has asked the locals to carry on with their activities and be cooperative to those soldiers.Rais Kikwete aliagiza operesheni hiyo ya kuwaondoa wahamiaji haramu ifanyike katika Mikoa ya Kigoma, Kagera na Geita kwa wakati mmoja ikisimamiwa na vyombo vya ulinzi na usalama yaani JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa na Uhamiaji akiwaonya wahalifu kuwa hapatakuwa na mahali pa kukimbilia wala kujificha.
President Kikwete has ordered that such an operation of repatriating (crackdown) on(of) illegal immigrants be conducted similtaneously in the provinces of  Kigoma, Kagera and Geita under TPDF (army), Police, secret services(intel) and immigration officers and warned criminals that they will not have a place to hide.
 
 
 
Huruma K. Nashimbi

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire