mardi 2 juillet 2013

Vikosi vya UN vya kulinda amani nchini Mali vyaanza rasmi majukumu yake

Kikosi cha usalama cha umoja wa mataifa UN
Kikosi cha usalama cha umoja wa mataifa UN
bbc.co.uk

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Mali, MINUSMA vimeanza rasmi jana jukumu la kuhakikisha usalama na utulivu wa nchi hiyo inayokumbwa na mgogoro, wiki nne tu kabla ya uchaguzi mkuu.

Katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika mjini Bamako kuashiria uanzishwaji wa MINUSMA Waziri wa Mambo ya Ulinzi Hubert Yamussa Kamara na waziri wa Mambo ya Nje Tieman Kulibaly, walihudhuria sherehe hiyo pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Herve Ladsous, na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Mali aliyemaliza muda wake Pierre Buyoya.

Vikosi hivyo vya takriban askari 12,600 vinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa Disemba na kuhakikisha usalama unarejea, hasa katika eneo la Kaskazini, sawa na theluthi mbili ya nchi ya Mali.

Ufaransa inakamilisha mpango wa kuwaondoa wanajeshi wake wapatao 4,500 ingawa wanajeshi wapatao 1,000 wataendelea kubaki nchini Mali ili kuendeleza jukumu la kusimamia usalama dhidi ya makundi ya kiislam.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire