mardi 2 juillet 2013

Barack Obama en Tanzanie: kunufaika na mradi wa umeme wa Marekani wa Power Africa

Rais Obama akiwa na mwenyeji wake Rais Kikwete
Rais Obama akiwa na mwenyeji wake Rais Kikwete
telegraph.co.uk

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Nchi za Bara la Afrika, Tanzania ikiwemo zinatarajia kunufaika na
mradi mpya wa Marekani unaojulikana kama Power Africa utakaowezesha
umeme kusambazwa mpaka kwenye maeneo ya vijijini.

Rais Barack Obama ametangaza kuanzishwa kwa mradi huo unaolenga kulisaidia bara la Afrika kuwa na umeme wa uhakika na ambao wananchi watamudu garama zake na kuahidi kuzijengea uwezo nchi hizo badala ya kutegemea misaada.

Amesema kuwa Marekani itaendelea kutoa misaada kwa bara la Afrika lakini suala la kujenga uwezo ni muhimu ili nchi hizo ziweze kujenga nchi zao kwa manufaa ya waafrika.

Kwa upande wake rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ameeleza namna ambavyo Tanzania imenufaika kutokana na misaada ya Marekani ambayo imesaidia ugonjwa wa Maralia kupungua kwa asilimia 50 huku umeme ukiongezeka na
kufikia asilimia 21.


Hii leo Jumanne Rais Obama anatembelea mradi wa umeme katika eneo la ubungo jijini Dar es Salaam ambao ameahidi kuongezea maradufu uwezo wa uzalishaji nishati hiyo.

Aidha rais Obama na  mtangulizi wake George W. Bush wataweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya watu waliouwawa wakati wa shambulizi la kigaidi kwenye ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire