Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani mjini Katanga, UN imeidhinisha kupelekwa kwa vikosi zaidi
UN Photo/Myriam Asmani
Kikosi hicho kitakuwa tayari kufanyakazi na Majeshi ya
Tanzania, malawi na Afrika Kusini yanayotarajiwa kuelekea Mashariki mwa
DRC ambapo Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa Herve
Ladsous anasema hatua hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa wananchi wa DRC.
Vikosi hivyo vinatarajiwa kuweoo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa muda wa mwaka mmoja lakini kuna uwezekano pia muda huo ukaongezwa kulingana na majukumu ambayo majeshi hayao yatakuwa nayo pamoja na hatua ambazo zitakuwa zimefikiwa kuwakabilia waasi.
Baraza la Usalama pia limeruhusu kutumika kwa ndege maalumu zisizo na rubani katika maeneo ya mpakani mwa nchi hiyo ndege ambazo awali nchi ya Rwanda ilipinga kutumika kwa kile ilichoeleza ni kushindwa kwa ndege hizo kule nchini Pakistan.
Operesheni nchini DRC imedhaminiwa na nchi za Ufaransa, Marekani na Togo ambazo zitahakikisha kikosi hicho mbali na kuwalinda wananchi dhidi ya uasi wa kundi la M23, pia kitakuwa na jukumu la kulinda usalama wa taifa ili kukabiliana a hatari zozote zitakazotishia Serikali halali ya nchi hiyo.
Kwa pamoja wajumbe wa UNSC wamelaani uwepo wa waasi wa M23 kwenye mji wa Goma na maeneo ambayo wanayashikilia wakiwataka waasi hao kuanza kujisalimisba wenyewe kwa wanajeshi wa Serikali kabla ya kukukabiliana na nguvu ya Jumuiya ya Kimataifa.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire